Asema kuwaachia Dk Shein, Maalim Seif pekee kutafuta mwafaka ni hatari
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wa Serikali iliyopita, Bernard Membe ameungana na waziri mwenzake wa
zamani, Dk Makongoro Mahanga kukosoa sera ya kubana matumizi
ya Rais John Magufuli ya kudhibiti safari za nje na kuteua baraza dogo la
mawaziri.
Kama ilivyokuwa kwa Dk Mahanga, waziri huyo aliyedumu kwa miaka tisa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje amesema kiuhalisia, Rais hajapunguza idadi ya wizara kama alivyosema bali amepunguza “idadi ya mifuko”, huku akisisitiza kuwa mkuu huyo wa nchi atalazimika kutoka nje “atake asitake”.
Membe amekuwa waziri wa pili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kukosoa sera ya kubana matumizi ya Serikali ya Awamu ya Tano baada ya Dk Mahanga, ambaye sasa amehamia Chadema, kumkosoa akisema idadi ya wizara inapimwa kwa kuangalia makatibu wakuu na si wizara na hivyo ukubwa wa Baraza la Mawaziri bado uko palepale.
No comments:
Post a Comment