Nikumegeeni kaufahamu kidogo tu ni kwamba,gari ikishauzwa na bima yake
inakufa automatically.Bima ni mkataba kati ya kampuni ya bima,na mteja
wa bima unaounganishwa na chombo chenyewe;yaani uhusiano wa kisheria
kati ya mteja wa bima na kampuni ya bima.Kwa mantiki hiyo,mmiliki wa
gari anapouza chombo maana yake amevunja uhusiano wake na shirika la
bima na mnunuzi mpya atalazimika kisheria kuanzisha uhusiano mpya na
shirika la bima,ikimaanisha kukata bima upya.Hii kwa kizungu inaitwa
kanuni/principle of insurable interest.hakikisha unafanya hivyo ili
kuepuka upotevu au hasara inayoweza kukupata kwa kutokujua.By Severe
I.M.-Shirika la bima la taifa(NIC)
No comments:
Post a Comment