Kwa mujibu wa sam sasali;Baada Ya Mch. Philemon Mollel Kusimamishwa kuendelea kuwa Mchungaji wa Usharika Wa Ngateu, Katika Dayosisi Ya Kaskazini kwenye Kanisa la KKKT kufuatia Kitendo chake Cha Kushinikiza Washirika wapatao 600,000 katika Dayosisi hiyo Wasichange shilingi 20,000 kila Mmoja ili kuokoa kupigwa mnada kwa Mali za Kanisa ikiwemo Hotel ya Kitalii Corridor Springs na Hospital ya Selian zilizokuwa zimewekwa rehani kufuatia deni la Kanisa hilo.
Katika Waraka Wake Pastor Mollel kwa waumini wote alitaka Washirika hao Wasichange fedha hizo zilizokuwa zimetolewa agizo na Askofu wa Dayosisi, mpaka pale waliosababisha kuchelewa kulipa deni hilo kufikia katika hatua hiyo ni kwa sababu ya Uzembe wa Watu Wachache. Alienda mbali zaidi alipodai kuwa ni Aibu kwa kanisa kama KKKT kutishiwa kuchukuliwa mali zake ili hali mpango wa urejeshwaji wa deni hilo ulishaazimiwa na baraza la Wachungaji Wa Dayosisi hiyo. Aidha alieleza kuchangisha fedha kwa waumini pasipo kutolewa maelezo na hatua kuchukuliwa hatua kwa waliosababisha uzembe huo ni kuufunika uzembe na mwisho wa siku makosa yale yale yatajirudia tena katika Dayosisi, lazima kuwepo na Uwajibikaji katika Jambo kubwa kama hilo.
Kufuatia waraka wake huo na maelezo yake Mch. Mollel alisimamishwa uchungaji wa Kanisa hilo katika Usharika wa Ngateu. Wiki Iliyopita Sharika 12 kupitia kikao Cha Halmashauri za Sharika hizo zimeazimia kwa Kauli Moja Hazitapeleka michango ya Kila Wiki Katika Dayosisi Ya Kaskazini Mpaka pale Pastor Mollel atakaporejeshwa katika Utumishi wake. Kwa Wastani Usharika Mmoja hupeleka kiasi cha 1.8 Mil Kila Wiki katika dayosisi ya Kaskazini ambayo ni sawa na 40% ya matoleo ambazo fedha hizo hutumika kwa ajili ya kuendeshea Ofisi ya Dayosisi. Sharika hizo 12 zimeazimia katika Kikao Cha Juzi Kati Kuto peleka fedha hizo mpaka pale Mch. Mollel arejeshewe utumishi wake.
Mgogoro huu unaokuwa pole pole kutokana na kuonekana kulindwa kwa watu fulani kufuatia deni hilo pasipo kuwajibishwa kwa kama ilivyokawaida ya Dayosisi Zote. Hata hivyo deni hilo la karibu Bilioni 11 liliokolewa na Wafanyabiashara 17 washirika wa KKKT Walionusuru Mali za Kanisa Kupigwa Mnada.

No comments:
Post a Comment