Kampuni ya simu ya VIETTEL inayotarajiwa kuanza huduma zake siku za hivi karibuni hana ncini,ni kampuni yenye asili Vietenam,na ni moja ya kampuni zinazokua kwa kasi kubwa sana hapa duniani.kampuni hii ambayo makao yake makuu yapo nchini Vietenam,ilisajiliwa rasmi mnamo tarehe 1 june 1989 ikianza huduma za mawasiliano rasmi mwaka 2000.Kwa sasa kampuni hii inaongoza nchini humo kwa kuwa na miundombinu bora na imara,na inatawala soko kwa zaidi ya asilimia 51 na ni kampuni pekee iliyofikia uwezo wa kuwafikia zaidi ya asilimia 86 wakati wa uzinduzi wake.Kuanzia mwaka 2005 hadi 2012 kampuni hii imakua ikipanda mara dufu kimapato,kwa mfululizo wa miaka saba
Kampuni hii kwa sasa inatoa huduma zake katika mataifa yasiyopungua saba yakiwemo ya Asia,america na Afrika na inasadikika kuwa inawafikia watu karibia milioni 170,ikiwa na wateja zaidi ya milioni 60. hadi mwaka 2012,pato la kampuni hii lilifikia kiasi cha dola za kimarekani 7 bilioni ikinufaisha zaidi ya walimu na wanafunzi wasiopungua milioni 27 katika mataifa husika na kwa kifupi,hii ndiyo kampuni pekee inayofikisha mawasiliano katika maeneo ya vijijini yasiyofikika kabisa.
Bloger alifanikiwa kuzungumza na maadhi ya maofisa wa kampuni hiyo ambao waliomba majina yao yahifadhiwe,katika mkoa mmoja hapa nchini.kwa mujibu wa maofisa hao hii ni kampuni ambayo inaingia hapa nchini kwa nguvu kubwa sana na kwa mtaji mkubwa sana.Kampunii kwa sasa inaendelea kujenga miundombinu yake katika mikoa yote hapa nchini na kwa mujibu wa maofisa hao,wamekuwa wakijenga minara hata katika maeneo mengi ambayo hayana mtandao wa mawasiliano kabisa.
Kampuni ya Viettel imewekeza zaidi kusambaza mtandao wao kwa teknolojia bora zaidi na kwa kutumia mkongo wa taifa yaani FIBER ambao unaaminika kuwa ndiyo mfumo pekee wenye nguvu zaidi katika kusafirisha mawimbi hapa nchini na ukiangalia unaweza ukajioneka kazi ya kuchimba mitaro pamoja na kufukia nyaya kuelekea kwenye minara mbalimbali ikiwa inaendelea katika maeneo mengi hapa nchini.
Kwa mujibu wa maofisa hao,kampuni hii itakuwa ikitoa huduma zake kwa gharama nafuu sana,na watasambaza ofisi zao ikiwezekana katika wilaya zote hapa nchini,pia wakiuza simu zenye teknolojia ya kisasa kabisa yaani smart phones kwa gharama nafuu sana hivyo kupelekea kampuni hii kutawala soko kwa kiwango kikubwa sana.
Habari hii imetolewa na Israel severe,the blogger.
Harrah's Cherokee Casino & Hotel - Mapyro
ReplyDeleteHarrah's Cherokee Casino & Hotel 구리 출장마사지 - Find your 군포 출장안마 way around the 서귀포 출장마사지 casino, find where everything 경기도 출장안마 is located 경주 출장마사지 with these helpful customer reviews:.