Zitto, Heche, Sakaya wazirarua,
Mtatiro ahoji watakaochaguliwa PAC kama wataweza kuvaa viatu vya ZZK
*Wabunge CCM wapongeza, mwingine
awaponda wapinzani awaita malofa
* Chenge, Aerukamba, Ghasia wapewa
uennyekiti wa kamati
Kitendo cha wabunge machachari wa
upinzani ambao wanasifika kwa uwezo wa kujenga hoja na kusimamia ukweli wa
mambo kutoswa katika Kamati nyeti za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu
za Serikali za Mitaa (LAAC) na badala yake wakajumuishwa kwenye kamati moja ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii, kimezidi kuibua mjadala mkubwa ndani na nje ya
Bunge.
Kuibuka kwa hali hiyo kunatokana na
kile ambacho wengi wamejenga hisia kwamba uongozi wa Bunge umefanya uteuzi huo
kwa kushirikiana kwa siri na Serikali ili kupunguza nguvu ya kambi rasmi ya
upinzani bungeni.
Wapo ambao wamekwenda mbali na
kuutupia lawama uongozi wa Bunge kuwa huenda umechukua uamuzi huo kwa shinikizo
la chama tawala cha CCM ambacho kipo katika mkakati maalumu wa kurejesha nguvu
yake ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 baada ya kuonja machungu
ya uchaguzi wa mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment