Tuesday, January 13, 2015

UTANDAWAZI KATIKA MTAZAMO WA UFALME WA MUNGU

Hapo mwamzo Mungu aliziumba mbingu na nchi,kisha akamuumba mtu tena kwa mfano wake wake,ili atawale na kumiliki.Adamu wa kwanza akawekwa kwenye bustani ya Eden,mahali palipojaa uwepo wa Mungu lkn pamoja na hayo alitenda  dhambi na Mungu akamwekea utaratibu mzuri tu ili asiangamie.Kizazi cha mwanadamu kiliendelea kukua,hata baadae dhambi iliendelea kutafuna ulimwengu na Mungu akaamua kushughulikia hili kwa njia ya gharika.

Mwanzo 11:
Wakati ule watu walikuwa na lugha moja,na usemi mmoja,watu wote walielewana na umoja na amani vilitawala.Kwa pamoja kwa kiburi na majivuno ya mwanadamu,wakaafikiana kujenga mnara mreefu(Babeli),ili wamfikie Mungu,na ndipo Mungu akachukizwa na kuamua kuwavurugha lugha ili wasielewane tena.Mungu akawasambaratisha katika maeneo mbalimbali duniani ili wasikae pamoja na kuwa kama walivyokuwa mwanzo.
Kutokea wakati huo mpaka sasa,ulimwengu uliendelea na kizazi cha mwanadamu  kiliendelea kukua,hata kufikia nyakati hizi za utandawazi.

Utandawazi ni nini?
-Turning the world into market economy(Kuurudisha ulimwengu kuwa wa uchumi huria).Kwa tafsiri hii,neno kuurudisha maana yaka wakati flani chumi za ulimwengu zilikuwa huru,lkn sasa zimefungwa.
-Kwa maana hii,maana tu ya neno utandawazi linatuthibitishia kuwa kuna wakati mambo yalikuwa huru lkn uhuru huo ulikoma,na kwa mawazo yangu,uhuru huu ulikuwapo kabla ya babeli.
-Kwa hiyo utandawazi ni mchakato wa kihistoria ulioanza na watu kuhama na kusafiri maeneo mbalimbali ulimwenguni,hasa kutoka bara letu la Afrika.Kwa kuhama au kusafiri karibu na hata mbali,wahamiaji,wenyeji na wengine walichukua mawazo,tamaduni,na hata bidhaa na kuzipeleka maeneo mengine.Kuigilizana,kuazimana na kuishi maisha ya watu wa jamii tofauti kukaanza kuonekana katika maisha ya watu.

Kwa hiyo utandawazi kwa maana hii ni kuunganisha chumi mbalimbali za ulimwengu mzima kupitia
-biashara
-Mzunguko wa fedha
-Mbadilishano wa teknolojia na mawasiliano,
-Mgawanyiko wa watu.
Mifumo ya biashara,fedha,teknolojia na mawasiliano na hata mgawanyiko wa watu vinamgusa kila mtu katika nyaja yeyote atakayokuwa na chini ya serikali yoyote hivyo,kila mtu atalazimika kuufuata na haiwezekani kuukwepa.
Kwa hiyo utandawazi ni matokeo ya kupanuka,kusambaa na kuimarika kwa biashara na mahusiano ya kifedha ulimwenguni.
-Utandawazi ni kama vile wakati wa babeli kw mfanano;kwa namna ambavyo dhambi inaendelea kuenea na kuutafuna ulimwengu,wanadamu wakijaribu kutafuta suluhisho la matatizo hayo bila kumshirikisha Mungu,Kwa kujaribu kurudisha ile nguvu,umoja na mamani waliyoitumia hata wakamuasi Mungu,kwa kuifanya dunia nzima kuwa kijiji,lugha moja,na usemi mmoja.
-Kumbuka awali nlikuambia kuwa kusudi la Mungu kutuumba sisi ni kuusimika ufalme wake hapa duniani,nasi tukitawala na kumiliki kwa niaba yake(koloni lake litawale),Yesu kristo akiwa mfalme pekee.
-Yesu kristo ni masiha chaguo la Mungu wa dunia nzima,na mpango huu wa kuufanya ulimwengu kuwa kitu kimoja unamweka pembeni bila kumhusisha kama vile hana umuhimu wowote ule.Alikufa msalabani kwa ajili ya ulimwengu mzima,na siku moja ulimwengu utamshuhudia akishuka ulimwenguni kama mfalme,na kila ulimi utakiri ya kuwa Yesu kristo ni bwana.
-Tayari utandawazi umeshika hatamu,huku dunia nzima ikielekea kwenda kutawaliwa na mtu mmoja,na tayari baadhi ya mataifa machache yanayotawala dunia yameanza kujichuja,na mpaka sasa wamebakia kama sita au saba,na kwa mujibu wa manabii ni lazima utafika wakati atabakia mmoja.Kwa maana hii ni wazi kuwa mwenendo wa ulimwengu huu unamuandaa mfalme mwingine ambaye si Yesu,kuja kutawala.

Danieli 2:44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele,wala watu wengine hawataachiwa enzi yake;bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu,nao utasimama milele na milele.

Math 24.
Chanzo cha matukio yote ni kurudi kwa mfalme wa kweli na wa haki(Yesu kristo) ambaye atakuta wenyeji  wa ulimwengu huu wameshasimika ufalme mmoja unaotawala ulimwengu mzima,dunia ikiwa kama kijiji,na ufalme huu ukiwa na matakwa yake binafsi kinyume na mapenzi  ya Mungu.
Suluhu ya Mungu juu ya uhasi huu uliopitiliza ni kuutikisa ufalme huo wa wanadamu(ulimwengu mzima),kwa matukio mbali mbali tena ya kutisha kama ilivyotabiriwa na manabii.

Danieli 12:1 “Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako,atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa.
Tukio la awali kabisa la utandawazi(amalgamation) lilionekana wakati wa babeli(Mwanzo 11)Siasa ya ujamaa na dini moja vilitawala kwa nguvu,utaratibu wote wa kuunganisha dunia nzima bila kujali wala kumshirikisha Mungu,wala maongozi ya Mungu.
Wengi tunamkumbuka mwanahistoria wa wakati huo Nimrod na jitihada nyingi alizozifanya wakati huo,katika kueneza ibada za miungu.

Kwa kuwa walikuwa kinyume na mpango wa Mungu ,Mungu aliamua kuugawa ulimwengu katika lugha tofauti na mataifa mbalimbali,Ili kuivunja nguvu yao ya umoja katika uasi.
Ulikuwa wakati maalum wa kutokomeza uasi na uovu uliokithiri,na kutengeneza njia kwa ajili ya mpango wake wa Masihi Yesu kristo,kurudi kuutawala ulimwengu na ndiyo maana ikaitwa babeli(Mwanzo 11:9).
Jitihada za sasa za kuunganisha ulimwengu bila Mungu zilitabiriwa na manabii ambao pia wametabiri uharibifu wake kwa kuja kwa Yesu kristo kuithibitisha hukumu ya msalaba.

Prophesies.
Tunaweza kuyathibitisha haya kupitia mipasuko mbalimbali ya mataifa makkubwa yaliyoungana na yenye nguvu,na  namna ambavyo kasi na shinikizo la mataifa kuungana inazidi kuwa kubwa.Mifano yake ni kama vileumoja wa ulaya,Mahakama ya kimataifa,Sheria za umoja wa mataifa zinazoondoa mamlaka ya sheria za ndanui za nchi mojamoja,Kubadili fikra za watu kuwa moja,mfumo wa kushirikiana sarafu moja unazidi kushika hatamu,
By.Israel Severe.

No comments:

Post a Comment

Ads 468x60px

Featured Posts