Friday, February 8, 2013

BABA ASKOFU THOMAS LAIZER WA KKKT AFARIKI DUNIA

Bado tukiwa na majonzi ya kumbukumbu ya kifo cha mama mzazi wa askofu Thomas Laizer,tuna wakati mgumu pia wa kuungana na familia ya marehemu Askofu thomas Laizer baada ya kifo chake kilichotokea katika hospitali ya rufaa ya Selian mjini Arusha alipokuwa amelazwa kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja. Namkumbuka baba askofu kwa mambo mengi hasa kwa tabia ya moyo wa kujali,tabia ambayo amekuwa nayo katika kipindi cha uhai wake hasa pale mtu anapokabiliwa na magumu. Nakumbuka mwezi Aprili mwaka 2011,alipodiriki kuahirisha maziko ya msiba wa mama yake aliyekuwa amefariki,na badala yake akaenda kumzika Mchungaji mstaafu wa kanisa hilo katika usharika wa Loruvani,Mchungaji Loakaki l.Severe bila kujali hali aliyokuwa nayo katika kipindi hicho kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na mama yake mzazi.Askofu huyu aliahirisha mazishi ya mama yake mzazi kwa ajili ya mazishi ya mchungaji huyu,na akaendelea na shughuli ya mazishi ya mama yake siku iliyofuata. Haya yametokea katika kipindi kigumu ambacho kanisa linaitaji sana uwepo na hekima yake,wakati kanisa hilo la KKKT likiwa katika mgogoro wa deni kubwa ambalo dayosisi hiyo ya kanisa la KKKT lilikuwa likidaiwa na benki mojawapo ya biashara mkoani Arusha.Katika hatua ya kuonyesha unyeyekevu na uwajibikaji,marehemu askofu Thomas Laizer alijishusha na kuliomba kanisa kushiriki kubeba mzigo huu kwa haraka kunusuru mali za kanisa zisipigwe mnada wakati wakiendelea na mchakato wa kuwajibisha Uongozi wa Hoteli inayomilikiwa na kanisa hilo,iliyosababisha hasara hiyo kubwa.

No comments:

Post a Comment

Ads 468x60px

Featured Posts