Tuesday, July 19, 2011

WATANZANIA SI MBUMBUMBU TENA.

Nina ujasiri mkubwa wa kulisema hili kwa sababu mimi pia ni Mtanzania, na sasa nimeyadhibitisha.Kwanza kabisa nguvu ya uma imekuwa kubwa sn hasa baada ya hamasa kubwa za upinzani.Ni wazi kwamba kulikuwa na mambo mengi hasa maamuzi yanayopitishwa na viongozi wetu hasa wa kiserikali,bila kuzingatia maslahi ya Watanzania wanaoumizwa hasa vitendo vya wabunge wengi wa chama tawala kupitisha hoja mbalimbali na maamuzi kishabiki.Hivi karibuni tumeshuhudia maneno `Thibitisha kauli yako´na`mwongozo wa spika´ jinsi yanavyotumika kwa nguvu na wabunge wa chama tawala kuwakatisha tamaa wapinzani.Chakushangaza sana ni kwamba kila palipoletwa kithibitisho(ushahidi),yanaisha kimya kimya.Nauliza hiki kimya maana yake imethibitika au vipi.Hata baadhi ya viongozi na wabunge wamekuwa wakiwadharau sn wapinzani na kuwaita wanafki wakati sisi watanzania tunashuhudia wenyewe wanavyotutetea.Mfano kuna kiongozi mmoja maarufu sana bungeni ambaye bila hata aibu,aliwaita wapinzani wanafiki kwa kile kinacholalamikiwa sana na wapinzani ambacho ni posho za wabunge.Sasa tumegundua nyingine mpya ya changizo la kuhakikisha mswada unapitishwa.Nauliza kuna maslahi gani huko mbona nguvu nyingi mno?Napenda kuwapongeza na kuwashukuru Chadema kwa kazi kubwa ya kuwazindua watanzania.Ukweli ni kwamba Watanzania si mbumbumbu tena,na kwa taarifa fupi tu ni kwamba siku hizi karibu kila mtanzania hata wale wasiozaniwa wanafuatilia maswala ya msingi hasa Bunge kwa karibu mno.Kwa hili,naamini sasa watanzania waliowengi kwa kufuatilia kwa karibu wanashuhudua wenyewe nani mtetezi,na nani adui.Nawasihi watanzania tusimame imara kwa kuisimamia wenyewe serikali yetu,ili tuvune mema ya nchi hii kwa pamoja kwa kuwa hatima ya wale wanaoipeleka nchi kubaya ipo mikononi mwetu sisi.Viongozi wote wajue kuwa sisi watanzania ndiyo wadau wakubwa wa nchi hii,na wazingatie kuwa tumewatuma na siyo kuwaneemesha.Kwa nguvu ya umoja wa uma;tuna uwezo wa kumuondoa yeyote tunayemuona hatufai,na kumuweka yeyote yule ambaye tunaamini ataweza kutuletea maendeleo.Kila Mtanzania asimame katika nafasi yake,na awajibike ipasavyo naana HAKI HUINUA TAIFA.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika,Amina.

No comments:

Post a Comment

Ads 468x60px

Featured Posts