Saturday, January 23, 2016

Marudio uchaguzi Zanzibar Machi 20



TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza kwamba uchaguzi wa marudio utafanyika Machi 20 mwaka huu na kuwataka wagombea wote walioshiriki katika uchaguzi uliofutwa wa Oktoba 25 mwaka jana, kujiandaa kushiriki uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha ametoa tamko hilo jana na kuongeza kuwa uchaguzi huo, utahusu nafasi ya Rais wa Zanzibar, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na masheha.
Akifafanua zaidi, Jecha alivitaka vyama vya siasa kujiandaa na uchaguzi wa marudio, ambao unatokana na uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana uliofutwa baada ya kujitokeza kwa kasoro mbali mbali ambazo zilibainisha wazi wazi kwamba uchaguzi huo usingekuwa huru na wa haki.
Kutokana na kasoro hizo ambazo zingeweza kuibua malalamiko mbali mbali zilizosababisha kufutwa kwa uchaguzi huo, Jecha aliwataka wagombea wote walioshiriki katika uchaguzi uliofutwa kujiandaa tena.
“Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) inawatangazia wananchi wote kwamba uchaguzi wa marudio utafanyika Machi 20 na hii inatokana na kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, baada ya kujitokeza wa kasoro mbali mbali ambazo ziliufanya uchaguzi huo sio huru tena,” alisema Jecha.
Aidha Jecha alisema kwamba katika uchaguzi wa marudio, hakutakuwa na uteuzi mwingine kwa wagombea wa nafasi zote ikiwemo urais, ujumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na masheha, bali watatumia wagombea wa uchaguzi uliofutwa.
Mbali na wagombea, Mwenyekiti huyo wa Zec pia alisema hakutakuwa na mikutano ya kampeni za uchaguzi kama ilivyokuwa kwa Uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/5713-marudio-uchaguzi-zanzibar-machi-20 

No comments:

Post a Comment

Ads 468x60px

Featured Posts