AMIRI Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli,
amesema nchi ipo salama na hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wala jeuri ya
kuleta chokochoko.
Amesema Jeshi la Ulinzi (JWTZ) liko imara na linatekeleza majukumu
yake ya kulinda mipaka ya nchi kwa uhakika na pia linashiriki kazi ya
kulinda amani katika nchi zenye migogoro.
Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana, katika kambi ya Jeshi ya Mbuni
iliyoko Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha, wakati akizungumza na
makamanda na wapiganaji wa kambi hiyo baada ya kuikagua Soma zaidi tembelea http://mtanzania.co.tz/?p=9933
No comments:
Post a Comment