Sunday, January 24, 2016
Gazeti la Habari Leo-Vigogo watatu NEMC wasimamishwa kazi
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, amewasimamisha kazi maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.
Maofisa hao ni Ofisa Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare, na Ofisa Mazingira, Boniface Benedict Kyaruzi.
Aidha, Waziri huyo ameagiza Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Bonaventura Baya, aandikiwe barua ya onyo kali na la mwisho kwa tuhuma ya udhaifu wa usimamizi wa watumishi wa NEMC, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza hilo.Kwa habari zaidi tembelea
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/5752-vigogo-watatu-nemc-wasimamishwa-kazi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment