25th January 2016
Simon Msuva ndiye aliyefunga goli la
kwanza la Yanga katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu waliposhinda 2-0 dhidi
ya Coastal Unioni Septmba 13 na jana akamjibu Mganda Hamis Kiiza wa Simba kwa
kufunga goli la kwanza la timu yake walipoichapa Friends Rangers mabao 3-0
katika mechi yao ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Taifa.
Kiiza ambaye pia alifunga goli la
kwanza la Simba katika ligi ya Bara msimu huu waliposhinda 1-0 dhidi ya African
Sports jijini Tanga Septemba 12, alitupia mara mbili wakati Wanamsimbazi
walipoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burkinafaso mjini Morogoro juzi.
Ushindi wa jana umeipeleka Yanga
raundi ya nne ya michuano hiyo ambayo bingwa wake ataiwakilisha Tanzania Bara
katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.
Msuva, Mchezaji Bora na Mfungaji
Bora wa ligi ya Bara msimu ulioita, alimjibu Kiiza kwa kufungua karamu ya mabao
ya timu yake alipotikisa nyavu kwa kichwa dakika ya tano baada ya kipenga cha
kwanza akiunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Issoufou Abubakar.Habari zaidi http://www.ippmedia.com/?l=88261
No comments:
Post a Comment