25th January 2016
Yadaiwa chanzo kudhibiti aibu kama
Richmond, Epa, Escow
Kasi iliyoonyeshwa na Bunge
lililopita katika kuisimamia Serikali kiasi cha kumlazimu Rais Jakaya Kikwete,
kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri zaidi ya mara nne, inatajwa kuwa
chanzo cha kuibuka kwa vita inayoonekana wazi ya kutaka kudhibiti mhimili huo
muhimu wa dola.
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati
tofauti jana, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa walisema mkanganyiko
ulioibuka kuhusiana na uteuzi wa kamati mbalimbali za chombo hicho ni ishara ya
wazi kwamba kuna vita ya kutaka kudhibiti utendaji wa chombo hicho, ambayo
mshiriki wake mkuu ni serikali ya awamu ya tano.
Wakieleza zaidi, baadhi ya
wachambuzi hao wamedai kuwa mwenendo wa Bunge la 11, kuanzia mchakato wake wa
kumpata Naibu Spika na hadi sasa katika uteuzi wa wajumbe wa kamati za Bunge,
unaashiria kuwa serikali imepania kupunguza makali ya chombo hicho ambacho
katika miaka kumi iliyopita kimejitahidi kwa kiasi kikubwa kutekeleza wajibu
wake wa kuisimiamia serikali kiasi cha kuibua masuala kadhaa yaliyotikisa
baraza la mawaziri, mfano ukiwa ni kashfa za Richmond, uchotwaji wa Sh. bilioni
133 za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) iliyokuwa Benki Kuu (BoT),
Operesheni Tokomeza na pia uchotwaji wa mabilioni ya fedha kupitia Akaunti ya
Tegeta Escrow iliyokuwa pia BoT.
Mwishoni mwa wiki, Spika wa Bunge,
Job Ndugai, alitangaza wajumbe wanaounda kamati mbalimbali za chombo
hicho huku mjadala ukiibuka kuhusiana na uamuzi wa kutowarejesha baadhi ya
wabunge walioitikisa serikali kutokana na kuibua kwao mambo kadhaa kupitia
kamati walizokuwamo. Wabunge wengi waliokuwa maaarufu wamejikuta wakikosa
nafasi katika kamati mbalimbali walizokuwapo awali ikiwamo nyeti ya Hesabu za
Serikali na Mashirika ya Umma (PAC), na kisha wengi wao kuwekwa katika Kamati
ya Huduma za Jamii.Kwa habari zaidi tembelea http://www.ippmedia.com/?l=88244
No comments:
Post a Comment