Monday, July 6, 2015

MAJANGA KWA YEYOTE ATAKAYESHIRIKI KUWAHARIBU WATOTO.

Tuachane na uhalifu mkubwa wa sasa kisiasa na kiuchumi hapa nchini hata tunaona mpaka wapinzani wanaopigania miswada isipitishwe kienyeji wanatolewa nje.Sakata la ESCRO pekeyake linatugarimu tozo katika mafuta na hataivo jumla ya makusanyo hayo tunayotozwa bila hatia hayafiki hata nusu ya fedha za eskro ikimaanisha ni lazima tubanwe maeneo mengine ili tuweze kuwalipia na kuwabeba hawa watu wachache.

Pia ufisadi ni eneo kuu mojawapo linalopelekea shilingi kishuka thamani na automatically mfumuko Wa bei(maisha magumu)

Nini hatma au dawa ya haya yote?Ni lazima tuwe na kizazi kipya chenye maadili,kitakachotunusuru na janga hili.Kama ni hivyo,wewe kama mzazi Wa sasa au mtarajiwa unayasimamiaje maadili ya mtoto katika familia na jamii inayotuzunguka.Ni kwanini unashiriki au kusupport madisco Toto na matukio mbalimbali yanayoharibu maadili mazima ya watoto?Hivi unajiskiaje unapozaa mtoto na mwishowe anaishia kua changudoa au shoga hasa kuanzia vyuoni mahali ambapo kama hujamlea vizuri,kumpenda na kumtahadharisha atajifunza kila aina ya uchafu?

Yesu anasema;ole wake yeye atakayeshiriki kuwaharibu watoto hawa...Ni kwanini umzalie shetani watoto?Si bora usingezaa kabisa!Ni wajibu wetu kujenga misingi ya taifa bora,takatifu litakalotokomeza anasa na uharibifu Wa kila namna.

Ni lini ulimbusu mwanao mara ya mwisho.Kama ni mambo ya kizungu ya kwako ya kinyaturu yako wapi?Ni lini ulimchukua mwanao ukamtabiria mafanikio na hata dua ya baraka kwa Mungu zaidi ya kumfananisha na shangazi au mjomba tena si ajabu ni mchawi una akili kweli!!!???.Ole wako(By Severe I.M.)

No comments:

Post a Comment

Ads 468x60px

Featured Posts