![]() |
Spika wa Bunge, Anna Makinda |
BUNGE limepitisha Mswada wa
sheria ya usimamizi wa mafuta na gesi ambao ulikuwa ukijadiliwa ambao
ulisababisha Spika Anna Makinda kuwatimua wabunge 46 wa upinzani. Anaandika
Dany Tibason … (endelea).
Mswada huo ambao
umepitishwa na wabunge wa CCM licha ya kuwa wachache, pamoja na mbunge wa
Wawi maarufu kwa jina la mbunge wa mahakama ,Hamadi Rashid
Mohammadi (CUF) .
Mbali na kupitishwa mswada huo Manaibu
Mawaziri wa Fedha Mwigulu Nchemba na Adam Malima,wametumia muda mwingi
kuwashambulia wabunge wa upinzani kwa kitendo chao cha kuondoka bungeni wakati
ikiendelea kujadiliwa bungeni.
Aliyeanza
kuwashambulia wabunge wa upinzani ni Mwigulu Nchemba ambaye amlitumia muda
mwingi kuwashambulia wabunge hao kwa madai kuwa wanakwamamisha maendeleo kwa
kutokubali kupitisha miswada ya mafuta na gesi.
Mbali na hilo
alitumia muda mwingi kujinadi kwa maelezo kwamba anasubiria kupitishwa kwa jina
lake la kuwania urais ili aweze kutekeleza sheria mbalimbali ambazo
zinapitishwa na bunge.
Amesema mambo ya
ajabu kuona baadhi ya wabunge wakiendelea kupinga upitishwaji wa miswada kwa
kutaka ipitishwe katika bunge lijalo.
Kwa upande wake
Malima amesema hakuna sababu yoyote ya wabunge kupinga miswada ambayo
wabunge wa upinzani wameipinga .
Malima kama ilivyokuwa kwa Mwigulu nae alitumia muda mwingi
kuwabeza na kuwadharau wapinzania ambao walikataa kupitisha mswada huo.
chanzo ni Mwanahalisi oline
No comments:
Post a Comment