Na Joyce Joliga,Mwananchi
Posted Jumapili,Novemba2 2014 saa 11:47 AM
Posted Jumapili,Novemba2 2014 saa 11:47 AM
Songea. Ni mwanamama mwenye vipaji lukuki na ambaye kwa kauli yake
anabainisha kuwa wanawake popote walipo wakikubali kushindwa ni lazima watashindwa
tena vibaya sana, lakini wakiamua kupambana hakuna kushindwa.
Huyu si mwingine ni Jacline Msongozi
ambaye ni Mama wa watoto wawili, kwake kushindwa siyo jambo rahisi, kwani
pamoja na kufanikiwa katika biashara ya upikaji wa vyakula pia ni Mwanasiasa ambaye
ana vyeo vingi zaidi katika Manispaa ya Songea.
Ameweza kupambana na ugumu wa maisha
kwa kujiingiza katika biashara mbali mbali ili aweze kutimiza ndoto yake ya
kuwa na Hoteli kubwa ya kitalii hapo baadaye.
Tayari diwani huyo wa Viti Maalumu
kupitia CCM ameweza kutoa ajira kwa vijana 37 kupitia biashara hiyo ambayo
imemsaidia kupata mafanikio. Kadhalika anajihusisha na ukulima katika mashamba
,ufugaji wa ng’ombe,mbuzi pamoja na samaki jambo ambalo limempa uzoefu na
mafanikio
Kuanza biashara:
Mjasiriamali huyo anaeleza kuwa
alianza rasmi biashara mwaka 1997 kwa kufungua saloon ya kike ambayo aliindesha
bila mafanikio , baadaye ajiingiza katika biashara ya kuuza mitandao ya simu za
TTCL, simu ,vocha na baada ya hapo akawa Wakala wa mitandao ya Tigo kwa wakati
huo ikijulikana kama Buzz.
Anasema, kutokana na kiu kubwa ya
mafanikio aliyokuwa nayo, aliamua kujikita katika biashara ya chakula, lakini
alikutana na changamoto nyingi kusafiri mara kwa mara ,bidhaa zilikaa hadi
kuharibika akaamua kwenda kufanya bishara ya kupika chakula kwenye sherehe.
“Naipenda sana biashara yangu ya
vyakula kwani imenisaidia kupata mafanikio makubwa sana nimeweza kujenga nyumba
bora ya kuishi eneo la Ruvuma, kununua usafiri pamoja na kupata mtaji wa
kununua mifugo kwa ujumla najivunia sana biashara hii,”alisema Jacline.
Anaongeza kuwa, kutokana na umahiri
wake wa mapishi amefanikiwa kupata tenda za zabuni katika
Akizungumzia alivyojiunga na siasa anasema alianza kujihusisha na siasa mwaka 2000 akiwa mkereketwa wa (CCM, ambapo aliingia umoja wa wanawake ,wazazi “Namshukuru Mungu nimepata mafanikio makubwa katika siasa, mwaka 2007 nilianza kugombea nafasi mbalimbali za ndani ya chama katibu mwenezi, mjumbe mkutano mkuu taifa mwaka 2007.
Mjumbe Halimashauri kuu kupitia UWT 2007 mjumbe kamati ya siasa (W)mjumbe kamati ya maadili (w)2008 nilichaguliwa kuwa katibu wa Elimu malezi,uchumi jumuia ya wazazi (w)songea mjini 2012 nilichaguliwa kuwa mjumbe baraza kuu wazazi Taifa 2013 nimeteuliwa kuwa mjumbe bodi ya maji (SOWASA)
Anasema, kutokana na kuwa na biashara pamoja na kiongozi wa siasa anajipangia ratiba ya kufanya mambo yake kila asubuhi ,kabla ya kujishusisha na mambo ya siasa anaweka taratibu za biashara zake kwanza baada ya hapo anaendelea na na vikao vya siasa
Wito kwa wanawake:
Anawataka wanawake wasiogope kupambana na maisha wajikite kwenye shughuli za ufugaji kilimo na ujasiriamali hasa ufugaji samaki ambao hauna gharama, Wajikite kwenye kilimo cha
mazao ufuta,alizeti kwani mazao hayo yana soko kubwa tofauti na zao la mahindi yanaleta usumbufu kwenye soko
Wanawake watambue kuwa wao ni wazazi, hivyo wajifunze kuwapenda na kuwasaidia watoto wao kwa kuwalea kwa karibu na kujenga malezi ya watoto,ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili.
No comments:
Post a Comment