Na Mwandishi wetu, Mwananchi
Pwani. Uongozi wa Kiwanda cha Kuchakata Asali cha Honey King,
wilayani Kibaha, mkoani Pwani, umeomba Serikali kupitia Kamati ya Bunge ya
Viwanda na Biashara, kuhakikisha wafugaji wa nyuki wanajengewa uwezo ili
kuzalisha asali bora.
Hatua hiyo itakiwezesha kiwanda
hicho kupata asali ya kutosha tofauti na sasa.
Akizungumza baada ya kamati hiyo kukagua kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu, Jack Liu alisema kiwanda hicho tangu kilipozinduliwa Juni mwaka jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hakijatimiza lengo lake la kuzalisha tani 10,000 za asali kwa mwaka.

Liu alisema hali hiyo inatokana na
kukosa asali bora ya kutosha kutoka kwa wafugaji nchini.
Alisema kuna mikoa mingi yenye asali, lakini wanapoichukua nyingi haina ubora, kwani baadhi ya wakulima huchanganya sukari guru, hivyo kulazimika kuagiza kiasi kidogo kutoka nchi jirani ili wasisimamishe uzalishaji.

Aliongeza kuwa anaamini iwapo
Serikali itawajengea uwezo wafugaji nyuki kwa kuwapa mafunzo au wataalamu
kutembelea mashamba yao mara kwa mara upo uwezekanao wa kupatika asali ya
kutosha.
Posted
Jumatano,Marchi20 2013
“Hatujazalisha kama tulivyolenga
wakati ule alipofika Waziri Mkuu hapa, maana tulilenga kuzalisha tani 10,000
kwa mwaka, lakini kumbe huko tulikotegemea kupata asali kuna changamoto kubwa
kwelikweli,” alisema Liu na kuongeza: “Naomba Serikali kutilia mkazo uzalishaji
wa kutosha wa asali, ili tukidhi mahitaji ya kiwanda ya kuzalisha tani
10,000.”
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani,
Mwantumu Mahiza alitoa taarifa ya hali ya mkoa huku aliweka wazi kuwa kiwanda
hicho tangu kuzinduliwa Juni mwaka jana hakijafanya uzalishaji wowote.
No comments:
Post a Comment