Monday, June 16, 2014

WAPE WATU SABABU YA KUMTUKUZA MUNGU KUPITIA MAISHA YAKO

TAFAKARI YA LEO Mioyo yetu na ifurike neno jema, ndimi zetu zikiwa kalamu mikononi mwa mwandishi stadi. Karibu tutafakari tena pamoja, Mt 5:14, sehemu ya 2: “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.” Umewahi kuingia hata siku moja ndani ya chumba chenye giza, ukawasha taa, giza likagoma kuondoka? Au likaomba ulipe kwanza dakika chache limalizie yake ndipo litoke? Biblia inasema, nuru inang’aa gizani, na giza kamwe haliwezi kuishinda (Yn 1:5) Nuru haiogopi giza hata siku moja, wala haijawahi kushindwa nalo. Cha kushangaza, sisi tuliopewa kuwa nuru, tunaogopa mara nyingi kuruhusu nuru yetu kuangaza. Tunawaza ‘watanionaje’? Tunataka tu kuangaza tukiwa kanisani; tukiwa na ‘walokole’ tu. Tunasahau kuwa impact ya nuru inaonekana zaidi sehemu yenye giza. Mara nyingi tumetafuta kufanana na watembeao gizani, ili watukubali, watupende, wasituchukie. Binafsi nilipokuwa sijaokoka, mlokole yeyote aliekuwa akifuata mienendo kama ya ambao hatukuwa tumeokoka nilimdharau sana. Hata leo hii, japo mtu atakushawishi uungane nae kutembea gizani, mwisho wa siku atakudharau tu. Acha nuru yako iangaze. Wape watu sababu ya kumtukuza Mungu kupitia maisha yako. UMEBARIKIWA! By B.Mrosso

No comments:

Post a Comment

Ads 468x60px

Featured Posts