Na Joseph
Zablon, Mwananchi
Jumanne,Marchi10 2015 saa 12:26 PM
Jumanne,Marchi10 2015 saa 12:26 PM
Kwa ufupi
Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Chai
Bora Kapila Ariyatilaka alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa bidhaa
zitokanazo na kahawa.
Dar es Salaam. Wakulima wa kahawa
nchini wataendelea kunufaika na zao hilo baada ya kuanzishwa kwa viwanda vya
usindikaji.
Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Chai
Bora Kapila Ariyatilaka alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa bidhaa
zitokanazo na kahawa.
Alisema wameingiza bidhaa mpya
sokoni zitakazopanua wigo wa soko la kahawa na kuwanufaisha zaidi wakulima.
“Tumekuja kupanua wigo wa soko la
kahawa, tuna mahitaji ya wastani wa tani 500 kwa mwezi, kwa ajili ya uzalishaji
wa bidhaa zetu hususan ile ya Cafe Bora,” alisema na kuongeza:
“Lengo la kampuni ni kutosheleza
mahitaji ya ndani pamoja na nchi za Afrika Mashariki.
Ariyatilaka alisema wakulima wa
nyanya, pilipili na bidhaa nyingine pia wana fursa nzuri ya soko baada ya
kampuni hiyo kuingia makubaliano ya kibiashara na Kampuni ya Dabaga iliyopo
Iringa.
“Tunaangalia zaidi fursa ya masoko
kwa bidhaa za mashambani kutokana na changamoto zinazowakabili wakulima, ndiyo
maana tunashirikiana na Dabaga,” alisema.
Alisema iwapo bidhaa za Dabaga
zitauzwa zaidi, mahitaji yataongezeka kwa wakulima wa nyanya Iringa na
kwingineko.
“Tutakuwa tumewawezesha wakulima
kuongeza kipato na pia Serikali itapata kodi zaidi kutokana na mauzo ,” alisema
Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa
Kampuni ya Chai Bora, Martin Ng’ethe alisema Tanzania inajivunia kuwa na aina
zote za kahawa.
Alizitaja kuwa ni Arabika na Robusta
tofauti na nchi nyingine zenye aina mmoja ya kahawa.
No comments:
Post a Comment