WIMBI la wizi wa kompyuta kwenye magari sasa limeshika kasi na wezi hao wamekuwa wakibadili mbinu kila kukicha.
Gari linaloonekana hapo limevunjwa kioo kwa namna yake na wezi hao waliokuwa katika gari aina ya Harrier ya Silver walifanikiwa kuchukua vilivyomo kwenye gari ikiwemo kompyuta ndogo maarufu kamakompyuta mpakato.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa nane mchana karibu na kituo cha mafuta cha Victoria.
Watu hao walikuja na kupaki gari karibu kabisa na gari hilo na wala huwezi kudhani kwamba wana nia mbaya kumbe hupulizia aina Fulani ya madawa ambayo hayajafahamika na kioo hupukutika hapo hapo.
Kitendo cha wizi huo kilifanyika ndani ya dakika moja au mbili kwani mwenye gari alikuwa jirani kabisa na gari lake na aliliona gari hilo likiwa karibu ila hakuwa na wasiwasi juu la jambo lolote lile. By Issa Michuzi.
MICHUZI: Tahadhari ya wizi wa kwenye magari
No comments:
Post a Comment