Saturday, February 9, 2013
MTOTO AFA MAJI SINGIDA
Mtoto mdogo wa darasa la tatu,amefariki dunia baada ya kutumbukia kisimani.Tukio hilo lilitokea jana jioni,nyumbani kwao Mwenge mkoani Singida.Hata vivyo kazi ya kuutooa mwili wake katika kisima hicho ilikuwa ngumu jambo lililopelekea mwili huo kukaa majini muda mrefu kutokana na kisima hicho kuwa kirefu.Mama mzazi alifikwa na wakati mgumu na wa huzuni sana kwani hii ni mara yake ya pili kufiwa na mwanae.Kwa mujibu wa majirani;miaka michache iliyopita,mama huyu almaarufu kwa jina la Mama Hasani,alifiwa na mwanae kichanga baada ya kuugua kwa muda mfupi.Bwana ametoa,Bwana ametwaa,Jina la Bwana lihimidiwe,Amina
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment