Sunday, January 20, 2013

MAONI MBALIMBALI JUU YA WEREMA KUKERWA NA BALOZI WA USWISS

Kama kawaida baada kupita katika vyanzo mbalimbali vya habari kuhusu habari ya CAG kukerwa na balozi wa Uswiss;nimeona nikuletee maoni mbali mbali kutoka vyanzo hivyo ili kukuwezesha kupata mtazamo wa watu mbalimbali juu ya hili.Hay ni baadhi tu ya maoni kutoka baadhi ya vyanzo vinavyoaminika kama nnavyonukuu. Ni aibu kwa viongozi wetu wakati wanapoambiwa ukweli na madudu wanayofanya,wanakasirika na kutaka kutoa visingizio ambavyo havina kichwa wala miguu. Huyo balozi wa uswiss yeye sio mjinga kuzungumzia hili tatizo.Tunawajuwa sana viongozi wetu na ukweli kila siku huwa unauma. werema kumbuka sasa hivi wananchi wameamka hawajalala kama wewe unavyofikiri. Hivi hachoki kuona aibu na madudu mnayofany-By Dickson Ngowi(Mwananchi) Huyu AG hana uweso na moyo wa kazi yake yeye ana mawazo mgado siku zote hamna siku aliongea jambo likawa anadhani mabalozi wa kizungu wanaongea uongo kuhusu nchi zao wewe pima tu maelezo ya balozi chave yana uzito kutaka pesa chafu zirudi tz huyu mpaka sasa hajui afanye nini ooh mara tume oh mara angekuwa balozi wetu angerudishwa oh kama mnawajua tupeni majina. bogus!! zitto alitaja majina yao yote, amesema mwanasheria mkuu ni nani kama sio yeye au chenge kuna aja kuuliza tena na tena-By Katumbwalala(Mwananchi) Jaji Werema hakusema chochote kyhuse mpango wa serikali,sasa ameona mtu kalifanyia kazi jambo hilo na yeye ndio anaanza kuongea,Jaji hacha tabia yako ya kusinzia wakati watu wanataka majibu-By Christois(Mwananchi). Hapa sasa na wewe umeomyesha weakness ya utendaji....Eti kama ingekuwa balozi wa TZ akasema haya Uswisi anagefukuzwa..ha ha ha ha...Sasa nyie mnashindwa nini kama amegusa mambo nyeti?Myerere aliwafukuza wangapi walionyesha dharau?Kama ni kweli unataka asiseme?BASI NA SISI TUMFUKUZE KWA KUINGILIA MAMBO YA TAIFA.By Baraka(www.wavuti.com) SASA KAMA HUKO USWISS ANGEFUKUZWA JE TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU CHA KUJIFUNZIA KUNYOA AIBU NI KAMA VILE SISI WOTE NI MITETEA NA JOGOO WETU NI BALOZI WA USWISS NI VEMA BALOZI HUYO ARUDI USWISS WALETE MWINGINE WAKITAKA NI VEMA TUDHIHIRISHE KUWA TUKO HURU SI TEGEMEZI KIASI HICHO-ASM(www.wavuti.com. Huyu WEREMA ni kichefuchefu kitupu. Hapa tunapata kuona umuhimu wa kumpunguzia madaraka Rais.. nchi kuwa na Attorney General kama huyu ni hasara kubwa. Huyu jamaa kazi yake ni kulipa fadhila kwa Rais kwa kazi yake aliyopewa..Huna hata aibu? Mwanasheria gani na ulisoma wapi wewe Werema? Hivi bado unafikiri waTanzania ni mbumbumbu? Hapana hatujalala... tunaelewa kinachoendelea huko serikalini.. Mwanasheria wa serikali anaomba wananchi waiombee serikali iweze kufanikiwa kurudisha pesa za nchi zilizofichwa? ...lol..kweli? Inaingia akilini kwa mtu hii? Halafu unasema balozi wa Uswis ni mtu mdogo? Je na pesa mnazoomba kwa ajili ya bajeti ya kila mwaka kutoka Uswis ni ndogo pia? Ebo...? We mzee muogope Mungu kabla ya shida zako...Wananchi wa Uswis wanatumia kodi zao kusaidia serikali ya Tanzania ambayo imejaa mafisadi na wewe ni mmojawapo kwa hiyo balozi anayohaki kuhoji serikali ya Tanzania. Tunafahamu fika mmekasirika kwa sababu mnataka kufunika hizi pesa.. Kama kweli mnafuatilia hizi pesa kwa nini iwe ni siri na kuomba muombewe dua? Wenye nchi wako tayari kuwasaidia sasa ugumu uko wapi? Hamtaki kwa sababu mtaumbuka, tunafahamu bora uendelee kunyamaza kuliko kuja kuongea utumbo.Hampendi kukosolewa wala kukumbushwa ndiyo maana mnang'ang'ania Rais aendelee kuwa na nguvu za kifalme:( Na wala usidanganye watu na demokrasia ya Uswis... Balozi anaweza kukosoa hapa na wala haijawahi kutokea kufukuzwa balozi hapa. Siku ipo utasimama mahakamani kujibu madhambi unayoyaficha kwa wanyonge waKiTanzania.By Anonymous said...(lukemusicfactory.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment

Ads 468x60px

Featured Posts