UAMSHO
Je! Ni laana au ni baraka?
(Sehemu ya Kwanza)
Hili
swali linakuja kwako – tena kwa wakati wake hasa! Nilikuwa nafundisha katika
kanisa fulani hapa nchini – nilipouliza swali hili wengi wakajibu kwa pamoja –
ni baraka! Lakini wakati huo huo walikuwako wazee wa kanisa ambao walikuwa
wanauona uamsho ya kuwa ni laana!
Nilipokuwa
nahubiri kwenye kanisa moja huko Marekani ya kaskazini – Mchungaji na wakristo
wa kanisa hilo walinieleza juu ya uamsho uliotokea kanisani hapo miaka michache
ya nyuma – na baada ya kipindi si kirefu kanisa likagawanyika na wakristo
wengine wakahama, wengine wakarudi nyuma kiroho. Nilipowauliza chanzo cha
mgawanyiko huo ni nini – wakajibu bila hata kusita, wakasema “Ni Uamsho!”
Je! unakubalina na jibu hili ya kwamba uamsho ukitokea katika kanisa huwa
unagawa wakristo?
Sehemu zingine vimetokea vikundi vya uamsho katika makanisa mbalimbali – mahali
pengine vimefurahiwa na mahali pengine vimechukiwa, hata kufika hatua hata ya
kuvipiga marufuku! Je! hii ni sawa?
Ni wakati gani uamsho unakuwa ni laana na ni wakati gani uamsho – unakuwa ni
baraka? Katika mfululizo huu wa maswali na majibu tutajifunza na kujibu maswali
mbalimbali kuhusu Uamsho.
Ni maombi yangu kwa Mungu ya kuwa mafundisho utakayoyapata katika majibu ya
maswali katika mfululizo huu yatakuimarisha zaidi katika maisha yako ya wokovu,
na katika kumtumikia Mungu.
Pia, ni maombi yangu kwa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo ya kuwa mafundisho
haya juu ya uamsho yatasaidia kutatua matatizo mengi yaliyopo katikati ya
Wakristo – hasa yanayotokana na uamsho.
Ndiyo maana ni vizuri hata wewe uyasome majibu haya ukiwa katika hali ya maombi
ili Mungu afungue moyo wako na akili zako upate kuyaelewa na maandiko. Maswali
tutakayojibu ni haya yafuatayo:
SWALI LA KWANZA: Uamsho ni kitu gani?
Ni rahisi sana kuchanganya maana za maneno na matukio yake, hasa tunapozungumza
juu ya Uamsho. Wengine wanachanganya maana ya uinjilisti na ile ya uamsho. Ni
budi ufahamu ya kuwa maneno haya Uinjilisti na Uamsho yana maana zinazotofautiana.
Neno ‘Uamsho’ limetafsiriwa toka kwenye neno la Kiingereza ‘revival’.
Na neno ‘revival’ linatokana na neno ‘revive’ ambalo lina
maana ya kuhuisha, kuchochea, kurudishia
nguvu, kufufua na kuamsha.
Kwa mfano Nabii Habakuki alipokuwa anaomba alisema; “ Ee Bwana, FUFUA kazi
yako katikati ya miaka …..” (Habakuki 3:2). Na katika Biblia ya Kiingereza
ya King James mstari huu umeandikwa hivi; “O Lord, REVIVE thy work in the
midst of the years …” kwa maneno mengine Nabii Habakuki alikuwa anaomba juu
ya uamsho.
Uamsho
unatokea wakati ambapo Mungu, kwa uweza wa Roho wake Mtakatifu anaposhuka ndani
ya mioyo au roho za watu wake ambao wamepoa, au wamerudi nyuma kiroho, au
wamekuwa vuguvugu au wamelala. Hawa watu mwanzo walikuwa wameonja nguvu
za Mungu, lakini baada ya muda walirudi nyuma kiroho au wakapoa. Uinjilisti
maana yake ni kuitangaza habari njema – au kutangaza habari za Yesu Kristo.
Uinjilisti hutumika wakati wa kuwaleta watu wasiookoka katika ufalme wa Mungu.
Uinjilisti ni matokeo ya Uamsho katika Kanisa. Kanisa lililopoa au kulala
kiroho huwa halina mzigo wa Uinjilisti wala wa kuleta mavuno ya roho za watu
kwenye ufalme wa Mungu.
Kwa kusisitiza tu ni kwamba Uamsho ni matokeo ya nguvu za Mungu kuwatembelea
upya WATU WAKE.
Nguvu za Mungu zinapowatembelea watu ambao hawajaokoka, na kuwafanya waokoke,
hatuliiti tendo hili kuwa ni uamsho, bali ni uinjilisti. Lakini nguvu hizi za
Mungu zinapowatembelea watu waliokwisha kuokoka tayari, na kuamsha upya kiu ya
kumjua na kumtumikia Mungu, huwa tunaliita tendo hili kuwa ni Uamsho.
Ndiyo maana ukienda katika madhehebu ambayo kuna wakristo waliookoka na ambao
hawajaokoka; wale waliookoka huwa mara nyingi huitwa ‘Wakristo wa uamsho’.
Ndiyo maana mara kwa mara unasikia maneno kama haya; mikutano ya uamsho, vijana
wa uamsho, watu wa uamsho, maombi ya uamsho, n.k.
Tunapozungumzia juu ya uamsho, ujue ya kuwa ni lazima kuna kitu cha kuamsha.
Kunakuwa na Uamsho, kwa kuwa kuna kitu cha kuamsha. Kunakuwa na ufufuko, kwa
kuwa kuna kitu cha kufufuka. Kunakuwa na kuhuisha, kwa kuwa kuna kitu cha
kuhuisha.
Kazi ya kuamsha roho za wakristo waliopoa, au waliorudi nyuma kiroho, au
waliolala kiroho, ni kazi ya Mungu mwenyewe, kwa uwezo wa Roho wake Mtakatifu.
Mtu aliyekuwa ameokoka akirudi nyuma na kufa kiroho, kazi ya kumfufua au
kumwamsha upya si ya mwanadamu bali ya Roho Mtakatifu.
Ingawa ni kweli kwamba Mungu humshirikisha mtu amtakaye katika kazi zake
mbalimbali kama tutakavyoona kadri tunavyoendelea; bado mwanzilishi na
msimamishaji wa uamsho ndani ya mtu ni Mungu mwenyewe.
Si vyema kumpa mwanadamu sifa ya kuleta uamsho mahali fulani, badala ya kumpa
Mungu ambaye amemtumia mtu huyo kama chombo tu.
Fahamu “si kwa uwezo (wa mwanadamu), wala si kwa nguvu (za mwanadamu), bali
ni kwa ROHO YANGU, ASEMA BWANA WA MAJESHI” (Zakaria 4:6)
SWALI LA PILI: Kwa nini Mungu analeta Uamsho?
Ukisoma katika Biblia utaona ya kuwa kuna sababu mbili kubwa ambazo zinamfanya
Mungu alete uamsho katikati ya watu wake.
Sababu ya Kwanza ni UAMSHO WA KAZI YA BWANA. Nabii Habakuki aliomba
hivi, “Ee Bwana, FUFUA KAZI YAKO katikati ya miaka; katikati ya miaka
tangaza habari yake; katika ghadhabu kumbuka rehema” (Habakuki 3:2).
Sababu ya Pili ni UAMSHO WA MIOYO YA WATU WA MUNGU. Mtunga Zaburi
aliomba hivi; “Je, hutaki kurudi na KUTUHUISHA (Kutuamsha), watu wako
WAKUFURAHIE? (Zaburi 85:6). Na katika kitabu cha Nabii Isaya 57:15
imeandikwa hivi; “Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye
jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo
patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili
kuzifufua roho za wanyenyekevu na kuifufua mioyo yao waliotubu”.
1. Uamsho wa kazi ya Bwana
“Ee Bwana, FUFUA KAZI YAKO katikati ya
miaka; katikati ya miaka tangaza habari yake; katika ghadhabu kumbuka
rehema” (Habakuki 3:2)
Nilipoyasoma maombi haya ya Nabii Habakuki nilijiuliza maswali kadhaa, na
baadhi yake ni haya: Je! kazi ya Bwana maana yake nini? Je! kazi ya Bwana nayo
inahitaji kufufuliwa? Kitu gani kinaua kazi ya Bwana hata ihitaji kufufuliwa?
Maswali haya yalinifanya nianze kukisoma kitabu cha Nabii Habakuki kwa makini.
Nilipokuwa nakisoma, niliyakuta mambo ambayo ningependa kukushirikisha hapa.
Kitabu cha Habakuki kwa sehemu kubwa kinaeleza mazungumzo kati ya Mungu na
nabii wake Habakuki. Habakuki anaanza kwa manung’uniko na malalamiko juu ya
uharibifu wa haki, na kutokuonekana kwa kazi au uwepo wa Mungu katikati yao.
“ Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia?
Nakulilia kwa sababu ya UDHALIMU, ila hutaki KUOKOA. Mbona
wanionyesha uovu, na unitazamisha UKAIDI? Maana UHARIBIFU NA UDHALIMU u mbele
yangu; kuna UGOMVI, na MASHINDANO yatokea. Kwa sababu hiyo SHERIA INALEGEA,
wala HUKUMU HAIPATIKANI; kwa maana watu wabaya huwazunguka
wenye haki, kwa sababu hiyo hukumu ikipatikana imepotoka” (Habakuki
1:2-4).
Ni wazi kwamba katikati ya wana wa Israeli – uzao wa Ibrahimu, kulitokea
UDHALIMU, UKAIDI, UHARIBIFU, UGOMVI, MASHINDANO, UVUNJAJI WA SHERIA, na
HAKI KUTOKUWEPO. Habakuki hakuona ya kwamba ni halali kwa mambo hayo
kuwepo katikati ya watu wa Mungu, na Mungu wao akae kimya.
Na Mungu alimjibu kuwa atalitumia kabila la Wakaldayo kuwaadhibu wana wa
Israeli (Habakuki 1:5 – 11)
Katika mahojiano yake na Mungu, Habakuki anakubali kabisa ya kuwa wana wa
Israeli wamekosa. Lakini anamwuliza Mungu ya kuwa kwa nini Yeye, aliye
mtakatifu, tena mwenye macho safi asiweze kuuona uovu huo (Habakuki 1:12 – 13),
na kwamba amewachagua Wakaldayo wapagani, ili watwae kisasi juu ya taifa teule.
Nabii Habakuki alitaka kujua kwa nini Mungu ameamua kuwaadhibu wana wa Israeli
kwa uovu wao kwa kuwatumia Wakaldayo walio waovu zaidi kuliko wao. Tena, kwa
nini amsaidie Mkaldayo aliye mjeuri asiye na haki, ili apate ushindi? Kwa
maneno mengine alitaka kufahamu kwa nini ujeuri, ugomvi na dhuluma vitawale
mataifa na si haki na amani?
Mungu alimpa Nabii wake Habakuki majibu mawili muhimu; 1. Mwishoni haki
itashinda;
2. “Mwenye
haki ataishi kwa imani yake” (Habakuki 2:4).
Baada ya mazungumzo hayo, ndipo Nabii Habakuki alipoomba sala hii “ Ee
Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka, katikati ya miaka tangaza habari
zake, katika ghadhabu kumbuka rehema” (Habakuki 3:2)
Kwa maneno mengine alikuwa anamwomba Mungu kuwa badala ya kuadhibu akumbuke
rehema ili awarehemu watu wake. Utendaji wa kazi yake ufufuke au uamke kwa upya
katikati ya watu wake. Palipo
na ugomvi alete amani. Palipo na dhuluma alete haki. Palipo na mashindano alete
ushirikiano. Palipo na ukaidi alete upole na unyenyekevu.
Je! huoni kuwa na sisi tunahitaji
kuungana na Nabii Habakuki kuomba juu ya uamsho wa kazi ya Mungu katika
makanisa na vikundi vya watu wa Mungu kama vya
maombi vilivyopoa? Katikati ya Wakristo kazi ya Mungu haionekani. Kumejaa
dhuluma, ukaidi, ugomvi na mashindano.
Wakati umefika wa wewe na
mimi kumwomba Mungu kwa juhudi ili kazi yake na matendo yake yaonekane tena
katikati yetu. Palipo na ugomvi atuletee amani ipitayo fahamu zote. Palipo na
mashindano atuletee ushirikiano katika Roho na kweli. Palipo na dhuluma
atuletee haki na hukumu za kweli zisizokuwa na upendeleo. Palipo na ukaidi
atuletee upole na kunyenyekea. Palipo na kuuchukia wokovu, alete kuupenda
wokovu. Palipo na uchovu na uzito wa kuifanya kazi ya Mungu, alete utayari na
wepesi badala yake! Kama ulikuwa hujaanza
kuomba, basi anza sasa kwa ajili ya mahali unapotaka mabadiliko yatokee kwa
wakristo wote kwa ujumla. Pia umwombe Mungu kuwa “katika ghadhabu akumbuke
rehema”.
2. Uamsho
wa mioyo ya watu wa Mungu
“Je! hutaki kurudi na KUTUHUISHA, Watu wako AKUFURAHIE?" Zaburi 85:6)
“Je! hutaki kurudi na KUTUHUISHA, Watu wako AKUFURAHIE?" Zaburi 85:6)
Tafsiri nyingine ya maneno
haya inasema hivi:
“Je hutatujalia tena maisha mapya
ili watu wako wakufurahie?”
Na katika maneno ambayo
Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake yanayozungumza juu ya FURAHA MIOYONI MWAO
– alisema hivi;
“Heri
ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa
uongo, kwa ajili yangu. FURAHINI NA KUSHANGILIA; kwa kuwa
thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi
manabii waliokuwa kabla yenu” (Mathayo 5:11,12).
Ukiona mtu aliyeokoka
anakosa amani na furaha wakati anaposhutumiwa, anapoudhiwa, na anaposingiziwa
uongo kwa sababu ya KUMWAMINI YESU, ajue ya kuwa amepoa kiroho na anahitaji
uamsho. Yesu alisema yanapotokea hayo FURAHI na KUSHANGILIA.
Pia, Yesu Kristo alisema hivi:
“
Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi;
ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa FURAHA. Mwanamke azaapo
yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki
tena ile dhiki, kwa sababu ya FURAHA YA KUZALIWA MTU ULIMWENGUNI. Basi ninyi
hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na MIOYO YENU ITAFURAHI, na
FURAHA YENU hakuna awaondoleaye. Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin,
amin, nawaambia, mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu. Hata sasa
hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata furaha yenu iwe timilifu
" (Yohana 16:20 – 24).
Furaha ya Bwana ndani ya mioyo
yetu sisi tulio wakristo, ndiyo nguvu ya kutuwezesha kuendelea katika wokovu
bila manung’uniko. Ukiona mtu anasema ameokoka na huku amekosa FURAHA YA BWANA
ndani yake, basi ujue kuna shida fulani katika maisha yake ya kiroho!
Katika kitabu cha matendo
ya Mitume furaha inaonekana wazi katikati ya wakristo hawa wa kwanza. Furaha inaonekana
walipopokea nguvu za Roho Mtakatifu (Matendo ya Mitume 13:52). Furaha
inaonekana Bwana alipofanya miujiza katikati yao (Matendo ya Mitume 13:8). Furaha
inaonekana katikati yao
walipoona watu wengine wakiokoka na kumfuata Yesu (Matendo ya Mitume 15:3). Na
pia furaha inaonekana walipokuwa wakiumega mkate (Matendo ya Mitume 2:46).
Na mtume Paulo katika
nyaraka zake kwa waumini anazungumzia furaha katika maeneo mawili muhimu. Kwanza, anazungumzia juu ya furaha aliyonayo anapowaona
wale aliowaongoza kwa Yesu wakiendelea katika imani ya wokovu (1Wathesalonike
2:19; Wafilipi 2:2). Pili, anazungumzia furaha anayopata yeye na mkristo yoyote
yule anapoteswa kwa ajili ya Kristo, kwa kuwa si furaha ya kibinadamu, bali ni
furaha iliyo tunda la Roho ndani ya mtu (Wagalatia 5:22).
Ni wazi kabisa ya kuwa Mkristo
asipoonekana ana FURAHA YA BWANA, basi hata maisha yake ya kiroho yanakosa
changamoto. Na wengine hufikia hata kuacha wokovu.
Nakumbuka wakati fulani mtu mmoja
alinifuata kwa ajili ya ushauri na akasema hivi; “Mimi nimeokoka, lakini naona napata mawazo ya kutaka
kuacha wokovu, na niliona kabla ya kufikia uamuzi huo nije kwako unishauri”
Mara moja nilifahamu ya kuwa
amekosa FURAHA katika njia hii ya wokovu. Baada ya kuzungumza na kumweleza kitu
cha kufanya kufuatana na maandiko, nilimwambia asiache wokovu. Nikamuuliza
“Ukimwacha Yesu utakwenda kwa nani? Namshukuru Mungu ya kuwa huyo mtu alipokea
ushauri niliompa na anaendelea na wokovu.
SWALI LA TATU: Uamsho ukitokea mahali kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu, mambo gani
yanatokea?
Uamsho unapotokea katikati
ya watu wa Mungu, kuna mambo mengi yanayotokea, lakini mambo makubwa yafuatayo
hujitokeza:
1. Hofu ya
Mungu
Palipo na uamsho pana hofu ya
Mungu. Kuna wakati unafika ambapo watu wa Mungu wanapoa na kutokujali sana mambo ya Mungu, na
kutokupenda maombi ya muda mrefu, na hata kufikia kutokwenda kanisani au kwenye
vipindi vya masomo ya biblia, kwa kujisingizia shughuli nyingi.
Ukiona mambo haya
yanajitokeza au yamejitokeza, basi ujue ya kuwa hofu ya Mungu haipo kati yao.
Na Mungu anapoamua
kujidhihirisha upya katikati yao
kwa uwezo wa Roho wake Mtakatifu, kunatokea uamsho, na uwepo wa Mungu unakuwa
wazi kwa kila mtu. Na palipo na uwepo wa Mungu, pana hofu ya Mungu.
Hofu ya Mungu inapotokea katikati
ya watu wa Mungu inaleta mambo mpya. Ikiwa umekaa na watu waliookoka utakuwa
umeona ya kuwa, hofu ya Mungu isipokuwepo katikati yao, huwa wengi wao wanaenenda bila ushuhuda
na bila hekima, na matokeo yake ni kuleta makwazo na kuufanya Wokovu udharauliwe.
Lakini hofu ya Mungu
inaporudi katikati yao
kwa sababu ya uamsho wa Roho Mtakatifu, wanaanza upya kutembea katika ushuhuda
na hekima. Je, unafahamu ni kwa nini? Kwa kuwa imeandikwa; “Kumcha Bwana
ndio mwanzo wa hekima, ……” (Zaburi 111:10).
Tafsiri nyingine ya hofu ya
Mungu ni kumcha Bwana. Mungu anapojidhihirisha upya katikati ya watu wake, kila
mmoja wao anaona kama vile Mungu ameshuka kwa
ajili yake tu na ameshuka kumshughulikia yeye tu! Kwa hiyo utaona watu wakiwa
wepesi kutubu dhambi zao na kutengeneza maisha yao ya kiroho.
Na kinachofuata ni watu hao
kuanza kujishughulisha upya na mambo ya Mungu. Utaona wanapenda utakatifu,
utaona wanapenda maombi na kumtumikia Mungu. Kunapotokea uamsho watu huona
Mungu yuko karibu nao zaidi kuliko alivyokuwa zamani.
Nakumbuka nilikuwa nahubiri
mahali fulani hapa nchini, na niliposema wale wanaotaka kutubu waje mbele, watu
wengi walikuja na kutubu kwa machozi, Roho wa Mungu alishuka kwa nguvu katika
mkutano ule.
Na nilipowafuatilia hao
waliotubu, nikaona ya kuwa robo tatu yao
walikuwa ni watu waliokuwa wameokoka zamani lakini wakarudi nyuma na kuanguka
dhambini. Na neno lilipohubiriwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, wakachomwa mioyo yao, wakawa kama watu
walioamshwa toka usingizini, wakaamua kutubu na kumrudia Bwana.
Na matokeo yake ni vikundi
vya maombi kuanza kwa upya; ‘Fellowship’ na kanisa kupata nguvu mpya, na watu
kushuhudia kwa ujasiri na bila woga. Hii si kazi ya mtu, ni kazi ya Roho
Mtakatifu aichunguzaye mioyo ya watu na kuijua ilivyo.
2. Watu
wengi wanaokoka
Watu wa Mungu wakipoa, hata
watu wanaozaliwa upya mara ya pili wanakuwa wachache. Watu wa Mungu wakiamka
upya kiroho, watu wengi wanaokoka. Ni wazi kwamba kunapotokea uamsho, mavuno ya
roho za watu yanakuwa mengi – kwa kuwa watu wanapata msukomo mpya wa
kushuhudia.
Hivi ndivyo ilivyokuwa
wakati wa wanafunzi wa kwanza wa Yesu Kristo.
Siku ya Pentekoste
ilipotimia. Roho wa Uamsho aliwashukia wale wanafunzi wa kwanza wa Kristo,
ambao walikuwa wamejaa hofu na wasiwasi; na baada ya kuwaamsha na kuwavika
ujasiri walianza kumsifu Mungu kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia
kutamka.
Uamsho huu katikati ya wanafunzi
wa Kristo, ulileta mafadhaiko na mshangao kwa wale ambao hawakuwa wanafunzi wa
Kristo. Imeandikwa: “Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika,
wakashikwa na fadhaa …. Wakashangaa wote ….” (Matendo ya Mitume 2:6,7).
Na wakati ule ule Petro
ambaye alikuwa amewahi kumkana Yesu Kristo mara tatu Roho Mtakatifu alimpa
ujasiri wa kusimama na kuhubiri kwa nguvu habari za Yesu Kristo.
Mtu aliyeamshwa na Roho Mtakatifu
akisema maneno yake huwa yamejaa moto ambao huwachoma wale ambao wanamsikiliza!
“Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo Yao,
wakamwambia Petro na Mitume wengine, Tutendeje ndugu zetu? Petro akawaambia,
tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo
la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, Kwa kuwa ahadi hii ni
kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote
watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Akawashu hudia Kwa maneno mengine mengi
sana na kuwaonya, akisema, jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao
waliolipokea neno lake (walioamua kuokoka) wakabatizwa na
siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu” (Matendo ya Mitume 2:37 –
41).
Kwa sababu ya uamsho wa
Roho Mtakatifu katikati ya watu wa Kristo, watu wengine ELFU TATU waliokoka kwa
siku moja na kwa mahubiri ya mtu mmoja, hii ni kazi ya Roho Mtakatifu!
Na hawa waliookoka si
kwamba walitubu na kutawanyika bali biblia inasema, “Wakawa wakidumu katika
fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate na katika
kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu …… Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa
wale waliokuwa wakiokolewa” (Matendo
ya Mitume 2:42 – 47).
3. Uamsho unaleta Umoja
Watu wa Mungu wakipoa
kiroho, matengano, magomvi na mashindano hutokea katikati yao. Watu wa Mungu wakipoa kiroho, huwa
wanapambana wao kwa wao badala ya kupambana na shetani.
Watu wa Mungu wakipoa
kiroho hata baraka za Mungu hazionekani katika makusanyiko yao, ndoa zao, na kazi zao. Wanakuwa ni watu
wanaoishi kwa kujitahidi, na siyo kwa nguvu za Roho Mtakatifu.
Imeandikwa hivi:
“Tukiishi
kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana
(Wagalatia 5:25 – 26)
“Tazama jinsi ilivyo vema, na kupendeza ndugu wakae pamoja, kwa UMOJA.………….. maana ndiko Bwana ALIPOAMURU BARAKA, Naam uzima hata milele” (Zaburi 133:1-3).
“Tazama jinsi ilivyo vema, na kupendeza ndugu wakae pamoja, kwa UMOJA.………….. maana ndiko Bwana ALIPOAMURU BARAKA, Naam uzima hata milele” (Zaburi 133:1-3).
Hii ni habari njema kusikia
ya kwamba BWANA AMEAMURU BARAKA ZAKE ZIENDE KWA WATU WANAOKAA PAMOJA NA KWA
UMOJA!
Ni kweli kwamba vitu vingi
vinaweza kutukusanya pamoja, kama vile ndoa,
harusi, misiba, mikutano, ibada, ugomvi, mashauri; nakadhalika. Lakini kuwa
pamoja haimaanishi kuwa mnao umoja.
Narudia tena: Lakini kuwa pamoja
haimaanishi kuwa mnao umoja. Mnaweza kuwa pamoja katika ibada au
harusi huku moyoni hampatani. Na hivi ndivyo ilivyo kwa watu wengi wa Kristo,
wanakaa au wanakutana pamoja lakini hawana Umoja!
Umoja wa kweli hauletwi na taratibu za kibinadamu hata kama ni nzuri sana. Zinaweza
kutufanya tuwe pamoja, lakini haziwezi kutufanya tuwe na umoja. Umoja wa kweli
huletwa na Roho Mtakatifu.
Ndiyo maana Roho Mtakatifu akijidhihirisha kwa upya katikati ya watu wa Mungu
huwa wanapatana na kuwa kitu kimoja bila kujali tofauti ya madhehebu yao!
Mipaka ya mapokeo ya kidhehebu, ya kikabila, ya kiutajiri, ya kimaskini, huwa
inavunjika!
Ndiyo ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Kristo wa kwanza walipohuishwa kwa uwezo wa
Roho Mtakatifu. Ukisoma katika kitabu cha Mtendo ya Mitume 2:41 – 42 utaona
jinsi wenzetu walivyoishi kwa Umoja.
Imeandikwa: “Nao waliolipokea
Neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa
wakidumu katika fundisho la mitume, na katika USHIRIKA, na katika kuumega
mkate, na katika KUSALI ……. Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na
kuwa na vitu vyote SHIRIKA wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa
navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. Na siku zote
kwa MOYO MMOJA walidumu katika hekalu, wakimega mkate NYUMBA KWA
NYUMBA na kushiriki chakula chao kwa FURAHA na kwa MOYO MWEUPE, wakimsifu
Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale
waliokuwa WAKIOKOLEWA”.
Kunapotokea uamsho, umoja wa kweli hutokea. Kulipo na
uamsho wa Roho Mtakatifu, ushirikiano wa kweli hutokea. Kunapotokea uamsho,
uchoyo unahama, ugomvi unahama, wivu unahama, uvivu unahama, na ubinafsi
unahama. Na tabia ya uamsho ni kuleta umoja wa kweli – watu waliopoa kiroho
wanaamka toka katika uchoyo, toka katika ugomvi, toka katika ubinafsi na wivu,
na badala yake wanaanza kushirikiana, kusaidiana, kupendana na kusali pamoja
katika Roho Mtakatifu.
Wakristo wenzentu wa mwanzo ndivyo
ilivyotokea kwao Roho Mtakatifu alipotawala maisha yao
na uhusiano wao – tunasoma hivi:
“Na jamii ya watu waliamini (waliookoka) walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali WALIKUWA NA VITU VYOTE SHIRIKA. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu miongoni mwao mwenye MAHITAJI; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile walivyouza, wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadri ya alivyohitaji” (Matendo ya Mitume 4:32 – 35)
Hata hivi leo maisha ya namna hii
yanatokea na ushirikiano wa namna hii unatokea ikiwa Roho Mtakatifu ataruhusiwa
kuleta uamsho kwa utaratibu wa Mungu wenye kuleta baraka na siyo utaratibu wa
kibinadamu au wa kishetani unaoleta laana
“Na jamii ya watu waliamini (waliookoka) walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali WALIKUWA NA VITU VYOTE SHIRIKA. Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu miongoni mwao mwenye MAHITAJI; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile walivyouza, wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadri ya alivyohitaji” (Matendo ya Mitume 4:32 – 35)
Amina hapa ni kwa neema ya bwana
ReplyDeleteGlory to God
ReplyDeleteNimeelewa mtumishi. Barikiwa sana
ReplyDeleteNeema ya Mungu iwe Juu yetu
ReplyDeletehili somo ni zuri sana , kwa viongozi wa makanisa na makundi mbalimbali ,kama tunahitaji mabadiliko tusome tena na tena.
ReplyDeleteasante mwalimu.
Amina na hakika
DeleteAmen, Amen!! Nimebarikiwa Sana na somo na Kuna kitu kimeongezeka ndani yangu! Mungu akubariki Sana baba
DeleteNmebarikiwa mno
DeleteNmebarikiwa mno
DeleteAmen, nimebarikiwa sana. Nimepata marifa
DeleteAmen,nimebarikiwa๐
ReplyDeleteNice subject Mwl
ReplyDeleteUAMSHO AGENDA YETU Nguvu Zaidi tunamtaka bwana na nguvu zake barikiwa sana mwalimu
ReplyDeleteAmen nimebarikiwa
ReplyDeleteAmen nimeelewa na nitalifanyia kazi kwa jina la Yesu
ReplyDeleteBarikiwaaaaaaaaaa Sana Mwalim
ReplyDeleteThank you mtumishi nimekuelewa na nimekubali na nimejifunza pia Mungu alie hai atusaidie
ReplyDeleteNimelewa.zaidi ya nifikirivyo ! Neno uamsho!/barikiwa sana Mwalimu wa neno LA Mungu.
ReplyDeleteNimeelewa sana ๐
ReplyDeleteMungu amenifundisha kupitia mafundisho haya mwalimu Mungu akupe neema ya kufika mbali.
ReplyDeleteMungu abariki na kuingilia kati kwenye vikundi na viongoz walioko makanisa tu ๐๐๐๐
ReplyDeleteNimekuelewa sana mtumishi wa Mungu ubarikiwe sana.
ReplyDeleteMungu aishie aendelee kukutumia zaidi sikuyajua haya
ReplyDeleteAmen babaangu
ReplyDeleteUbarikiwe zaidi
ReplyDeleteKila nikisoma hii huwa napata nguvu mpya,Mungu akubariki sana mtumishi wa Mungu
ReplyDeleteHallelujah
ReplyDeleteMungu akubariki mwl kwa SoMo zuri na Mungu anipe kuliishi
ReplyDeleteasante mumishi wa MUNGU kwa mafundisho hayon mazuri.
ReplyDeleteNashukuru mno kukutana na hekima ya mwl. Hakika nimejifunza vitu vingi Katika somo hili. Barikiwa mno baba
ReplyDeleteMungu akubariki Sana mtumishi wamungu kwasomo zuri nimeelewa sana
ReplyDeleteAmina nimebarikiwa saana nami nitafundisha somo hili kanisani
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteAmeen ubarikiwe mtumishi wa Bwana๐
ReplyDeleteAmina
ReplyDeleteAmeen ๐ nimetoka na kitu kipya leo
ReplyDelete