DAKTARI Willibrod Slaa – Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), amesema uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa Biometric
Voters Registration (BVR) ni mchezo wa kisanii. Anaandika
pendo Omary….(endelea).
Mfumo huu unatumika kuchukua au kupima
taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia za mwanadamu na kuzihifadhi katika
kazidata (database) kwa ajili ya utambuzi.
Dk.
Slaa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kurejea kutoka
nchini Marekani alikokwenda kwa ziara ya siku 10 akiwa ameongoza na mkewe
Josephine Mshumbusi.
“Mchezo
wote wa BVR ni usanii. Nimetoka Marekani, huko wana umeme saa 24. Wana huduma
ya simu saa 24. Lakini hawatumii mfumo wa BVR katika chaguzi zao,” amesema Dk.
Slaa.
Aidha, amesema “Taarifa ya Mtaalam kutoka Marekani ni kwamba, BVR
inaashiria yanayofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni ya makusudi.
Inajua kuna wananchi hawataandikishwa. Ndio maana wameanza uandikishaji katika
ngome za Chama cha Mapinduzi (CCM).
Dk.
Slaa ameongeza kuwa, mbali na BVR kuwa mchezo wa kuingiza, pia ni ufisadi ambao
umegharimu mabilioni ya fedha za walipa kodi.
“Tenda
ya BVR ilikataliwa na Mamlaka ya Kusimamia Manunuzi ya Umma (PPRA). Hakuna
mchakato wowote wa wazi wa zaburi uliofanyika,” amesema.
Akiwa
nchini Marekani, Dk. Slaa ameweza kuzungumza na wawekezaji ambao wako tayari
kushirikiana na Tanzania. Hatua hiyo ni katika kukuza uchumi wa Taifa
utakaonufaisha maisha ya Watanzania.
“Wenzetu
wako tayari kushirikiana na sisi. Wapo tayari kuwekeza kwa masharti yetu.
Chadema haina ugomvi na wawekezaji. Lakini hatuhitaji wawekezaji wezi, mafisadi
na wanaoingia mikataba ya siri na serikali. Hatuko tayari kuona mtu anakuja
anachota rasilimali zetu,” amesema Dk. Slaa.
Katika
ziara hiyo, pia ametembelea miradi kadhaa ikiwemo ya ufugaji wa ng’ombe wa
maziwa na miradi inayoendeshwa na vyuo vikuu ambapo amesema Tanzania inahitaji
teknolojia, nyezo za kazi na ujuzi ili iweze kupiga hatua katika maendeleo.
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments:
Post a Comment