Thursday, January 3, 2013

MOTO MKUBWA WATEKETEZA MADUKA SINGIDA

Moto huo ambao chanzo chake hakikuweza kujulikana maramoja,uliteketeza maduka pamoja na stoo za wafanyabiashara kadhaa na kusababisha hasara kubwa,majira ya saa tano asubuhi leo.Cha ajabu na kushangaza ni kwamba,pamoja na ajali za mara kwa mara za nyumba kuungua moto hapa mkoani Singida,bado gari la moto ni lilelile dogo sana,na liko moja tu katika mkoa wa Singida.Pamoja na hayo,gari hili lilichelewa sana na kufika katika eneo la tukio wakati moto umeshateketeza kabisa maduka hayo,cha ajabu zaidi hata maji yaliyokuwa katika gari hilo yalikuwa ni kidogo sana.
Kama inavyoonekana katika picha hii ni nyumba inayomilikiwa na shirika la nyumba la taifa NHC nyumba namna 3-G sokoni road,Singida.
Baadhi ya wakazi na wasamaria wema wakifanya jitihada za kuuzima moto huo.
Hii ni sehemu mojawapo ya nyumba hiyo,iliyoharibiwa vibaya sana na moto huo.
Usemi usemao kufa kufaana unathibitika hapa;baadhi ya wakazi wakijaribu kuchota mchele uliomwagika kwa wingi.
Hii ni mojawapo ya babashop maarufu sana mjini Singida,iliyoathiriwa vibaya na moto huo..

No comments:

Post a Comment

Ads 468x60px

Featured Posts